Sunday, 24 April 2016

KOFFI OLOMIDE NA KIFO CHA PAPAA WEMBA


Asubuhi ya Jumapili April 24 2016 ndio zimeanza kusambaa taarifa za kifo cha mwimbaji Mkongwe kutoka Congo DRC aitwae Papa Wemba ambaye imeripotiwa amefariki baada ya kuanguka jukwaani akiwa anatumbuiza huko Ivory Coast.
Taarifa za kifo zimeendelea kuwafikia watu mbalimbali akiwemo mwimbaji mkongwe wa Congo DRC Koffi Olomide ambaye ameandika maneno machache kwenye ukurasa wake wa Instagram akisema ‘kwaheri Kakaasante‘ na kuambatanisha picha yao ya pamoja ya siku nyingi kwenye hayo maneno.
Koffi Olomide amekua akitajwa kuwa mpiga gitaa wa zamani na mtunzi wa nyimbo kadhaa zilizoimbwa na Papa Wemba.
Koffi 2
KWA HISANI YA MILLARD AYO.COM

Saturday, 30 January 2016

AMIRI JESHI NA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI WA KIJESHI JWTZ

VIDEO: Maamuzi ya Rais Magufuli kwa Mkuu wa Majeshi Mwamunyange: http://millardayo.com/mwamunyange3016/

Hii ni aibu kwa Taifa letu

British helicopter pilot 'shot dead by Tanzania poachers' - http://www.bbc.co.uk/news/uk-35450490

Wednesday, 13 January 2016

ODM CONDEMS GOVERNMENT OVER ATTEMPTS TO REGULATE RELIGIOUS ORGANISATIONS

http://citizentv.co.ke/news/odm-condemns-govt-over-attempts-to-regulate-religious-organisations-111635/

Thursday, 31 December 2015

NI MABADILIKO UTEUZI WA MAKATIBU WAKUU NA MANAIBU



mtz1* Magufuli ampeleka Maswi TRA
* Majenerali JWTZ wapewa wizara nyeti
RAIS Dk. John Magufuli amemteua Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Eliakimu Maswi, kuwa Kaimu Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kutengua uteuzi wa aliyekuwa anashika wadhifa huo, Lusekelo Mwaseba ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Kabla ya uteuzi huo, Maswi alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, lakini alisimamishwa kutokana na tuhuma za uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow, kabla  ya kusafishwa na tume iliyoundwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete na kuteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Manyara.
Mbali na uteuzi huo, Rais Magufuli amefanya uteuzi wa makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu katika wizara mbalimbali, huku akiwaacha makatibu wakuu kadhaa.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Dar es Salaam jana, ilisema katika uteuzi huo, Rais Magufuli ameteua makatibu wakuu 29 na naibu makatibu wakuu 22.
Katika uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Balozi Ombeni Sefue kuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Peter Ilomo, Katibu Mkuu Ikulu na Dk. Laurian Ndumbaro, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora.
Katika Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhandisi Mussa Iyombe ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Dk. Deo Mtasiwa (Naibu Katibu Mkuu – Afya) na Bernard Makali (Naibu Katibu Mkuu – Elimu).
Ofisi ya Makamu wa Rais, Katibu Mkuu ni Mbaraka Wakili na naibu wake ni Mhandisi Ngosi Mwihava.
Rais Magufuli amewateua makatibu wakuu watatu katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu) ambao ni Erick Shitindi (Katibu Mkuu Kazi na Ajira), Mussa Uledi (Katibu Mkuu Bunge) na Dk. Hamis Mwinyimvua (Katibu Mkuu – Sera).
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi pia ameteua makatibu wakuu watatu ambao ni Dk. Frolence Turuka (Katibu Mkuu – Kilimo), Dk. Mashingo (Katibu Mkuu Mifugo) na Dk. Budeba (Katibu Mkuu – Uvuvi).
Kwa upande wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, itaongozwa na Mhandisi Joseph Nyamuhanga (Katibu Mkuu – Ujenzi), Dk. Leonard Chamuliho (Katibu Mkuu – Uchukuzi), Profesa Faustine Kamuzora (Katibu Mkuu – Mawasiliano) na Mary Sassabo (Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano).
Taarifa hiyo imesema Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi itaongozwa na Katibu Mkuu, Dk. Yamungu Kayandabira na naibu wake, Dk. Moses Kusiluka, wakati Wizara ya Maliasili na Utalii itaongozwa na Katibu Mkuu Meja Jenerali Gaudence Milanzi na Anjelina Madete (Naibu Katibu Mkuu).
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji itakuwa na makatibu wakuu wawili, ambao ni Dk. Adelhem James Meru (Katibu Mkuu – Viwanda) na Profesa Adolf Mkenda (Katibu Mkuu – Biashara na Uwekezaji) ambaye naibu wake ni Mhandisi Joel Malongo.
Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, itaongozwa na Katibu Mkuu Maimuna Tarishi akisaidiwa na naibu makatibu wakuu wawili, Profesa Simon Msanjila na Dk. Leonard Akwilapo, huku Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, itaongozwa na Katibu Mkuu Afya, Dk. Mpoki Ulisubisya.
Kwa upande wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, makatibu wakuu ni Sihaba Nkinga na Profesa Elisante Ole Gabriel Mollel, huku Nuru Mrisho akiteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu.
Katika Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Mbogo Futakamba amebaki kwenye nafasi ya Katibu Mkuu na naibu wake ni Mhandisi Kalobero Emmanuel.
Wizara ya Nishati na Madini imepata mabadiliko baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu, Omar Chambo kuondolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Profesa Justus Ntalikwa, huku akisaidiwa na manaibu Profesa James Mdoe na Dk. Paulina Pallangyo.
Wizara ya Katiba na Sheria, Katibu Mkuu wake ni Profesa Sifuni Mchome, akisaidiwa na manaibu wawili, Suzan Mlawi na Amon Mpanju.
Kwa upande wa Wizara ya Mambo ya Ndani itaongozwa na Katibu Mkuu Jaji Meja Jenerali Projest Rwegasira na naibu wake ni Balozi Hassan Yahaya.
Wizara ya Fedha na Mipango imeachiwa Katibu Mkuu yule yule Dk. Silvacius Likwelile ambaye sasa atakuwa na manaibu watatu ambano ni Dorothy Mwanyika, James Dotto na Amina Shaban, wakati Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Katibu Mkuu ni Dk. Aziz Mlima na naibu wake ni Balozi Ramadhan Mwinyi.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Katibu Mkuu wake ni Job  Masima  na naibu wake ni  Immaculate Peter Ngwale.
Taarifa hiyo ilisema makatibu wakuu na naibu makatibu wakuu wote ambao wameachwa katika uteuzi huo watapangiwa kazi nyingine.
MASWI
Kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 250 ilisababisha Maswi aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini asimamishwe mwishoni mwa Desemba mwaka jana.
Mbali na Maswi, aliyekuwa waziri wake, Sospeter Muhongo pia alisimamishwa pamoja na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.
Mei mwaka huu, Balozi Sefue alibainisha kuwa uchunguzi uliofanywa kuhusu tuhuma za Maswi kuhusika kwenye sakata la akaunti ya Tegeta Escrow, umebainisha hana hatia na hajahusika kwa namna yoyote kwenye kashfa hiyo.
Alisema uchunguzi huo umeonyesha hakuna ushahidi wa moja kwa moja uliomtia hatiani Maswi, Profesa Muhongo na mawaziri wengine wanne ambao waliong’olewa na Bunge baada ya majina yao kutajwa katika kashfa ya Operesheni Tokomeza.
Aliongeza kuwa Maswi alikuwa akichunguzwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Kamati ya Uchunguzi wa Awali ya Mamlaka ya Nidhamu ambazo zote hazikumkuta na hatia wala ukiukwaji wowote wa maadili ya viongozi wa umma.
Ripoti za uchunguzi huo zilibaini alichokifanya Maswi kilizingatia matakwa ya sheria, ushauri wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ridhaa ya Shirika la Umeme nchini (TANESCO), hivyo hakuna kosa linaloweza kumfanya afunguliwe mashtaka ya kinidhamu akidaiwa kuruhusu utoaji fedha zilizokuwa katika akaunti hiyo.
Balozi Sefue alisisitiza kuwa Maswi alitenda kazi yake kwa kiwango kinachoridhisha kwa kufanya mawasiliano na mamlaka mbalimbali kwa nyakati tofauti na hakuwa miongoni mwa watu waliopata mgawo wa fedha au fadhila yoyote.
Alisema Profesa Muhongo naye hana hatia kwani wakati Maswi akichunguzwa, naye walikuwa wakimchunguza ndiyo maana kuna baadhi ya watu walipelekwa kwenye Baraza la Maadili kuhojiwa, lakini yeye hakupelekwa.


IMETOKA MTANZANIA

BILIONI 500 ZAHITAJIKA KUSAMBAZA DAWA NCHI NZIMA

Mkurugenzi Mtendaji wa MSD, Laurean Bwanakunu
Mkurugenzi Mtendaji wa MSD, Laurean Bwanakunu

BOHARI Kuu ya Dawa nchini (MSD) imedai kuwa licha ya Serikali kuilalamikia kwamba hushindwa kupeleka dawa za kutosha katika vituo vya afya na hospitali za wilaya na mikoa, imedai kikwazo kinachosababisha kukosekana kwa dawa ni bajeti ndogo. Anaandika Moses Mseti, Mwanza … (endelea).
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa MSD, Laurean Bwanakunu, wakati wa uzinduzi wa Duka dawa la jumla na rejareja, uliofanyika katika hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou Toure, mjini hapa.
Amesema ili vituo vya afya na hospitali ziweze kupata dawa na kufanya kazi yake kwa ufanisi na dawa za kutosha ziweze kupatikana kwenye hospitali hizo za Serikali inahitajika Sh. 577 bilioni.
Bwanakunu amesema kuwa Serikali imekuwa ikiilalamikia MSD kwamba imekuwa ikishindwa kusambaza dawa katika hospitali za Serikali huku ikishindwa kutambua tatizo bajeti inayotengwa.
“Sasa hivi vituo vya afya na hospitali za Serikali zinapokea bajeti ya Sh. 80 bilioni lakini kiasi hicho hakitoshi kabisa na ili huduma itolewe ya uhakika na dawa ziweze kupatikana inatakiwa Sh. 577 bilioni.
“Rais (Dk. John Magufuli) ameahidi kuongeza bajeti katika wizara ya afya kufikia kiasi cha Sh. 577 bilioni, tunatarajia sasa kiasi hicho kitaweza kupunguza ama sio kumaliza kabisa tatizo la dawa hospitalini,” amesema Bwanakunu.
Hata hivyo amesema licha ya ukusanyaji wa mapato kuwa mkubwa katika hospitali za mikoa na vituo vya afya nchini lakini kiasi cha bajeti kinachotengwa hakilingani na ukusanyaji huo wa mapato.
Pia amesema kufunguliwa kwa duka hilo kubwa katika mkoa wa Mwanza, litaweza kuhudumia hospitali za mikoa ya kanda ya ziwa na kuweza kupunguza tatizo la ukosefu wa dawa hospitalini.
Meneja wa MSD kanda ya ziwa, Byekwaso Tabura, amesema duka hilo limeghalimu kiasi cha Sh. 27 milioni na litakuwa linauza dawa za kila aina na ambazo zilikuwa hazipatikani hospitalini.

MWANAHALISI FORUM

MAANDALIZI YA KUTANGAZWA MAALIM SEIF YAIVA ZANZIBAR

Mgombea wa Urais Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim SEif Shariff Hamad
Mgombea wa Urais Zanzibar kwa tiketi ya CUF, Maalim SEif Shariff Hamad


USHINDI wa Maalim Seif Shariff Hamad katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25, ungali salama. Anaandika Jabir Idrissa … (endelea).
MAWIO limeelezwa kuwa ushindi huo utadhihirishwa kabla ya Zanzibar kufikia kilele cha maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi.
Taarifa zinasema viongozi wa kitaifa, wakiwemo marais wastaafu Zanzibar, ambao wamekuwa wakikutana na Maalim Seif, Ikulu ya Zanzibar, wanakaribia kukamilisha utaratibu wa kuwezesha kiongozi huyo kutangazwa mshindi wa uchaguzi huo.
“Hili halina utata wowote. Nakuhakikishia wanakaribia kuona mantiki na kuelewana; utaratibu wa kumtangaza Maalim Seif utatolewa wakati muafaka,” amesema mwanadiplomasia kutoka moja ya mataifa ya Ulaya.
Amesema kwa kadri anavyofahamu, maendeleo ya mazungumzo hayo yanayomhusisha pia Rais Dk. Ali Mohamed Shein, katika siku za karibuni, yamejikita katika kupata uhakika kuwa serikali mpya itaundwa kwa kuzingatia matakwa ya sheria na katiba.
Lakini amesema, hata suala hilo halijawa tatizo kwa kuwa mfumo wa kuunda serikali umesukwa vema katika Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984.
“Kama unavyojua mfumo wa serikali utakuwa uleule wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kwa matokeo ya uchaguzi vyama vya CCM na CUF ndivyo vitaunda serikali mpya,” alisema.
Mwanabalozi huyo aliulizwa na mwandishi jinsi anavyoona hali ya kisiasa kwa sasa na hasa kuhusu mgogoro uliotokana na uchaguzi.
Mgogoro wa sasa Zanzibar ulitokana na uchaguzi mkuu kufutwa kiubabe na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.
Jecha alifuta uchaguzi kwa tangazo lililorushwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) mchana wa Oktoba 28.
Wakati huo tayari Jecha alikuwa ameshatangaza kura za majimbo 33, akibakiza majimbo 21 tu.
Mwandishi alilenga kupata msimamo wa Jumuiya ya Kimataifa kuhusu kauli tata za viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar, Waride Bakari Jabu aliwataka wana-CCM kujiandaa kwa uchaguzi wa marudio aliosema utafanyika “wakati utakapowadia.”
Hata hivyo, kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya habari ndani ya CCM, Serikali ya Mapinduzi na Serikali ya Muungano, hakutakuwa na uchaguzi wowote bali utakuwepo utaratibu wa kumtangaza mshindi.
Chanzo katika CCM kimesema, “Hili liko wazi, mshindi wa uchaguzi ule ni Maalim Seif wa CUF ambaye naweza kusema amefanikiwa kusimamia ushindi wake huo na hoja zake hazishindiki. Nakwambia atatangazwa siku chache zijazo.”
Kiongozi huyo ambaye aliomba asitajwe jina gazetini, amemsifia Maalim Seif kwa kubaki mtulivu wakati wote akijadiliana na viongozi wenzake ambao wote ni kutoka CCM.
Katibu Mkuu huyo wa CUF na mwanasiasa ambaye amekuwa akilalamika kuhujumiwa mara zote akigombea urais, amekuwa akishiriki mazungumzo na marais wastaafu.
Marais hao ni Ali Hassan Mwinyi, Dk. Salmin Amour Juma, Amani Abeid Karume na Dk. Shein. Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi naye amehudhuria mazungumzo hayo.
Dalili za kuwepo muafaka katika majadiliano zimeonekana hivi karibuni pale Dk. Shein, aliyekuwa akigombea urais kwa mara ya pili, na Maalim Seif walipokutana na Rais mpya wa Tanzania, Dk. John Magufuli katika nyakati tofauti.
Wote walisikika wakisema majadiliano yao yanaendelea vizuri, lakini Dk. Magufuli akieleza waandishi wa habari nje ya ofisi yake Ikulu baada ya kukutana na Maalim Seif kuwa, “amenihakikishia wanaendelea vizuri na nimemtaka wakamalize majadiliano yao na apige kazi.”
Dk. Shein alipotoka nje ya maongezi na Dk. Magufuli aliwaambia waandishi wa habari kuwa mazungumzo yanaendelea vizuri na yatakapomalizika, watatoa taarifa kwa umma kuwaeleza maafikiano yaliyofikiwa.
Taarifa zilizopatikana baadaye zinasema moja ya mambo ambayo Dk. Shein alitakiwa kuyafanya baada ya hapo, ni kukutana na Kamati Maalum ya NEC-CCM, kuwaeleza maendeleo ya vikao na viongozi wenzake vinavyofanyika Ikulu.
Jumapili iliyopita, MAWIO lilielezwa kile kilichotokea katika kikao kilichofanyika Ofisi Kuu za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar kilichoandaliwa kwa ajili ya Dk. Shein kutoa taarifa yake.
Katika kikao, Dk. Shein “alitoa taarifa yake na taarifa yenyewe kujadiliwa vizuri” mpaka kikao kilipomalizika yapata saa 9.30 alasiri.
Dk. Shein aliondoka na Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, mara baada ya kumaliza kikao.
Lakini baada ya viongozi hao wakuu kuondoka ukumbini, baadhi ya wajumbe waliobaki walianza kudai kuwa hawakubaliani na mapatano na kwamba wanataka uchaguzi urudiwe.
Gazeti hili limeambiwa baada ya Dk. Shein kuondoka Kisiwandui, Balozi Seif alifuatana na baadhi ya viongozi kwenda Ofisi ya Mkoa wa Mjini Magharibi, iliyoko Amani, ambako walifanya mjadala ulioibua kilichoitwa “kauli za chuki” zikimlenga Maalim Seif.
Kwa kuzingatia aliyoyasema Dk. Shein, baadhi ya viongozi walionekana wakifuta machozi kwa kilichoelezwa ni “kutoamini kwao kuwa CUF itapishwa kuongoza serikali mpya.”
Akijibu hoja ya kurudia uchaguzi ambayo wananchi wengi wameonesha kuipinga, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano na Umma wa CUF, Ismail Jussa Ladhu amesema kurudia uchaguzi siyo chaguo la wananchi.
Aliwaambia waandishi wa habari mgogoro wa Zanzibar ni wa kutengeneza, uliolenga kuchanganya wananchi na kuwapora ushindi wao. Ametaka wananchi wapuuze kauli za kurudia uchaguzi.
“CUF inawahakikishia Wazanzibari kwamba haitotetereka; itasimamia kwa dhati maamuzi waliyoyafanya kwa njia za kidemokrasia kupitia uchaguzi mkuu na italinda chaguo lao la Rais wa Zanzibar, Wawakilishi na Madiwani wao,” alisema Jussa.
Amepongeza wananchi kwa kuonesha “ukomavu wa hali ya juu wa kisiasa na kuendelea kutunza amani na utulivu wakati wakisubiri matokeo ya kazi kubwa waliyoifanya tarehe 25 Oktoba ambayo inaashiria ujenzi wa Zanzibar Mpya.”
Ni msimamo wa CUF kuwa Maalim Seif alishinda uchaguzi kwa zaidi ya kura 25,000.
Kwamba CUF ilipata viti 27 vya uwakilishi. Kwamba CCM ilishindwa kupata kiti kisiwani Pemba. Kwamba CUF ilitwaa viti tisa Unguja
MWANAHALISI FORUM,