Saturday, 21 November 2015

MH.MAJALIWA KASSIMU MAJALIWA NDIE WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

                                                       Mhe.Majaliwa Kassim Majaliwa
                                             WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO
                                                                            WA
                                                                    TANZANIA



Hatimae Magufuli ametegua kitendawili cha nani ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,ni baada ya kumpendekeza kwa Bumge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mbunge wa Lwanga Mhe.Majaliwa Kassimu Majaliwa katika nafasi hiyo.
Bunge limethibitisha uteuzi huo na Mhe.Majaliwa Kassimu sasa ndie Waziri Mkuu wa 11 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hii hapa mi orodha ya Watanzania waliowahi kukalia nafasi hiyo tokea tumepata uhuru kutoka kwa Muingereza mwaka 1961.

Waziri Kiongozi wa Tanganyika
Jina Amechukua Ofisi Ameondoka Ofisini Chama
Julius Kambarage Nyerere 2 Septemba 1960 1 Mei 1961 TANU
Mawaziri Wakuu wa Tanganyika
Julius Kambarage Nyerere 1 Mei 1961 22 Januari 1962 TANU
Rashidi Kawawa 22 Januari 1962 9 Desemba 1962 TANU
Nafasi Zilizoondolewa Tangu (9 Desemba 1962-17 Februari 1972)
Mawaziri Wakuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Rashidi Kawawa 17 Februari 1972 13 Februari 1977 TANU
Edward Moringe Sokoine 13 Februari 1977 7 Novemba 1980 CCM
Cleopa David Msuya 7 Novemba 1980 24 Februari 1983 CCM
Edward Moringe Sokoine 24 Februari 1983 12 Aprili 1984 CCM
Salim Ahmed Salim 24 Aprili 1984 5 Novemba 1985 CCM
Joseph Sinde Warioba 5 Novemba 1985 9 Novemba 1990 CCM
John Malecela 9 Novemba 1990 7 Desemba 1994 CCM
Cleopa David Msuya 7 Desemba 1994 28 Novemba 1995 CCM
Frederick Sumaye 28 Novemba 1995 30 Desemba 2005 CCM
Edward Ngoyai Lowassa 30 Desemba 2005 7 Februari 2008 CCM
Mizengo Pinda 9 Februari 2008 19 Novemba 2015 CCM

No comments:

Post a Comment